Haba na haba hujaza kibaba
Sijui kwanini lakini hivi karibuni nimeikumbuka sana methali ya “haba na haba hujaza kibaba.” Nafikiri nafahamu sababu. Akili yangu inapenda kujihusisha na mambo kadhaa kwa wakati mmoja, lakini katika hii miaka ya karibuni sikufanya kazi kwa mfumo ambao unaufaa ubungo wangu. Najikuta nahitaji mapumziko ya muda mrefu baada ya wiki au miezi kadhaa.
Suluhisho nililofikia ni kufanya kazi kidogo katika kila jambo linalonivutia liwe kusoma kitabu, kujifunza lugha, au kujenga kitu fulani. Nafanya maendelo zaidi nikitumia mbinu hii. Njia hii inalazimu subira sana sana wakati wa mwanzo ambapo kila kitu kinaokana kigumu na huna uhakika kama unasonga mbele. Inaweza ikachukua miezi mpaka mwaka kuona matundo ya kazi yako, usikate tamaa, kazaa buti na endelea na kazi. Mimi ni shahidi kwamba njia hii inafanya kazi.